Wahamiaji halali wanapata huduma za afya katika manisapaa sawa na wazawa wa Ufini. Vipimo vya afya kwa wahamiaji ...
Manispaa yote nchini Ufini yanatoa huduma za afya kwa wenyeji wake, kwa kawaida kila manispaa yana kituo chake ...
Vituo vya afya hufungwa wakati wa jioni na wikendi. Vituo vinapofungwa magonjwa sugu hutibiwa katika vituo vya ...
Kama sehemu ya huduma za afya manispaa huwapa wenyeji wake taarifa na huduma zinazohusu ujauzito. Akina mama ...
Kama mwenyeji wa manispaa una haki ya kutumia huduma ya umma ya matibabu ya meno. Manispaa hutoa huduma za ...
Nchini Ufini, daktari hutoa maagizo ya dawa ya ugonjwa. Utapewa maagizo ya daktari ambayo utapeleka katika duka la ...
Kama mwenyeji wa manispaa una haki ya kupata bima ya maisha nchini Ufini. Bima hii ina huduma na mafao ...
Mhamiaji ana haki ya kutuma maombi ya kujiunga na Mfumo wa Shirika la Bima ya Maisha la Ufini. Fomu za kujiunga hujazwa ...
Taarifa kuhusu mafao ya bima ya maisha inapatikana katika ofisi zako za Kela na katika ofisi za ustawi wa jamii za manispaa ...
Wahamiaji halali wanapata huduma za afya katika manisapaa sawa na wazawa wa Ufini. Vipimo vya afya kwa wahamiaji wote halali na jamaa zao hufanywa wanapowasili katika manispaa yao mapya. Kutakuwa na mkalimani vipimo vya afya vinapofanywa. Wakati wa mahojiano, muuguzi atakupima magonjwa yote ambayo umewahi kuugua, dawa ulizotumia na chanjo ulizopata. Kumbuka kubeba rekodi za daktari na matibabu uliyopokea. Huduma zinazopatikana katika kituo cha afya, kuweka miadi na namna ya kulipa zitaelezewa. Nchini Ufini, madaktari wote wanatakiwa na sheria kuweka siri.
Manispaa yote nchini Ufini yanatoa huduma za afya kwa wenyeji wake, kwa kawaida kila manispaa yana kituo chake cha afya. Kama mwenyeji wa manispaa nchini Ufini una haki ya kutumia huduma za afya za manispaa. Weka miadi ya kuonana na daktari au muuguzi unapoumwa kwa kutembelea au kupiga simu kwenye kituo cha afya. Subiri miadi yako katika ukumbi wa kusubiri wa kituo cha afya.
Vituo vya afya hufungwa wakati wa jioni na wikendi. Vituo vinapofungwa magonjwa sugu hutibiwa katika vituo vya afya vya dharura. Vituo hivi huwa katika hospitali za mkoa. Katika hali ya kuhatarisha maisha mtu anapaswa apige simu nambari ya dharura ya 112.
Kama sehemu ya huduma za afya manispaa huwapa wenyeji wake taarifa na huduma zinazohusu ujauzito. Akina mama wanashauriwa watembelee daktari kupimwa katika kituo cha afya cha manispaa kabla ya mwezi wa nne wa mimba haujaisha. Afya na kukua kwa mtoto hupimwa katika kliniki ya wajawazito. Akina baba wanahimizwa kuandamana na mama mjamzito kwenda kliniki ya wajawazito wapate mafunzo ya kutunza mimba. Kwa kawaida watoto huzaliwa katika hospitali ya mkoa iliyo karibu katika manispaa yako. Akina baba wanaweza kuwepo mama anapojifungua.
Kama mwenyeji wa manispaa una haki ya kutumia huduma ya umma ya matibabu ya meno. Manispaa hutoa huduma za matibabu ya meno katika kliniki za meno.
Nchini Ufini, daktari hutoa maagizo ya dawa ya ugonjwa. Utapewa maagizo ya daktari ambayo utapeleka katika duka la dawa kununua dawa yako. Kama unaugua ugonjwa sugu, kumbuka kubeba rekodi zako za hospitalini unapoenda kumwona daktari nchini Ufini.
Kama mwenyeji wa manispaa una haki ya kupata bima ya maisha nchini Ufini. Bima hii ina huduma na mafao mbalimbali katika hali tofauti za maisha. Shirika la Bima ya Maisha la Ufini (Kela), hutoa huduma zake kwa wenyeji wote wa manispaa katika masuala ya jamii.
Wahamiaji halali wanaruhusiwa kupata bima ya maisha sawa na Wafini halisi.
Kama huna ajira, unapaswa kutafuta ajira kwa bidii na kujiasili na Ofisi ya Ajira na Maendeleo ya Uchumi (TE) kama anayetafuta kazi ndiposa uwekwe kwenye mpango wa kutanganama. Baada ya hapo, utaweza kulipwa mafao ya kukosa kazi.
Mtu asiyeweza kupata ajira kwa sababu ya hali yake ya kimaisha kama vile ugonjwa wa muda mrefu, ulemavu au ujauzito, anapaswa kuomba mafao yanayofaa. Mtu aliyezidi umri wa miaka 65 na alieyeishi nchini Ufini kwa muda wa miaka mitatu, anaweza kupata pensheni ya Kela.
Mafao ya kulipa gharama za maisha hutumiwa pia nchini Ufini. Haya mafao huwezesha watu wote waweze kuishi maisha bora. Mtu anaweza kuomba mafao ya kulipa gharama za maisha kama mafao mengine hayatoshi kulipa gharama za kila siku. Mafao ya kulipa gharama za maisha yanaweza kupungua mtu anapopata mshahara au mafao mengine ya kutosha.
Mafao yote huombwa kwa ofisi ya Kela.
Mhamiaji ana haki ya kutuma maombi ya kujiunga na Mfumo wa Shirika la Bima ya Maisha la Ufini. Fomu za kujiunga hujazwa katika ofisi za Kela zilizo karibu. Baada ya uanachama kuidhinishwa mhamiaji atapokea kadi yake ya bima ya jamii inayomwezesha kutuma maombi ya kupata mafao ya jamii kutoka kwenye ofisi za Kela. Mafao haya ni kama mafao ya familia, kusoma, kukosa kazi, ulemavu na pensheni ya kustaafu. Mwanachama hutuma mwenyewe maombi ya kupata mafao ya Kela na mafao haya hulipwa katika akaunti yake ya benki.
Taarifa kuhusu mafao ya bima ya maisha inapatikana katika ofisi zako za Kela na katika ofisi za ustawi wa jamii za manispaa yako na kwenye tovuti ya Kela. Manispaa mengi huandaa maonyesho ya kutoa habari kuhusu huduma za manispaa na mafao ya bima ya maisha kwa wahamiaji wageni. Ni muhimu kwa mhamiaji kuhudhuria maonyesho haya ili kupata taarifa ya kutosha. Mashirika yanayoshirikiana na wahamiaji na wahamiaji ambao wameishi nchini Ufini kwa kipindi kirefu wanaweza pia kusaidia wahamiaji wapya kwa masuala yanayohusu maisha ya kila siku na huduma za bima ya maisha.
Pakua hapa yaliyomo katika kurasa huu katika muundo wa PDF.