Utapata taarifa ya msingi kuhusu jamii na maisha ya kila siku kwenye tovuti hii, kadhalika msamiati wa msingi wa lugha ya Kifini. Tovuti hii imeundwa mahsusi kwa wahamiaji halali wanaokuja nchini Ufini.
Ufini iko Kaskazini mwa dunia katikati ya Uswidi na Urusi. Ufini inapakana na Norwe upande wa Kaskazini. Upande wa Kusini Ufini inapakana na Estonia. Soma zaidi.
Wewe ukiwa mhamiaji halali pamoja na uliowaandika katika barua yako ya maombi, mmepewa hali ya wahamiaji, kibali cha kuishi cha kudumu na haki ya kufanya kazi nchini Ufini. Soma zaidi.
Safari ya kwenda Ufini hufanyika angani hutumia ndege. Safari huanza katika Uwanja wa ndege. Kwa sababu kila abiria anaruhusiwa kusafiri na mzigo wa kilo 20 ni muhimu kuchagua vitu utakavyosafiri navyo na utakavyoviacha. Soma zaidi.
Kama mhamiaji halali wewe na familia yako mnastahiki kupata nyumba ya kuishi katika manispaa utakayoishi. Ukubwa wa nyumba na idadi ya vyumba katika nyumba yako itategemea idadi ya wakazi, lakini vifaa vya kimsingi katika nyumba ya kuishi havitabadilika. Soma zaidi.
Watoto wengi ambao hawajafikisha umri wa kwenda shuleni nchini Ufini husajiliwa kwenye shule za chekechea za kutwa kwa sababu wazazi wengi hufanya kazi mbali na nyumbani. Kama mkazi wa manispaa, unaweza kutuma maombi ya nafasi ya mwanao. Soma zaidi.
Ni muhimu kukumbuka kwamba lugha ya kazini nchini Ufini ni Kifini. Kuna sehemu chache sana za kazi ambazo lugha ya kazi ni Kiingereza. Lazima usome Kifini ili uweze kuajiriwa nchini Ufini. Soma zaidi.
Wahamiaji halali wanapata huduma sawa za afya na ustawi wa jamii sawa na wananchi wengine wa Ufini. Uchunguzi wa afya unaandaliwa kwa wahamiaji wote halali na familia zao wanapowasili katika manispaa yao mapya. Soma zaidi.