Maisha ya Kila Siku

Ghorofa ya Kupangisha

Kama sehemu ya msingi ya wahamiaji, wewe na familia yako mnastahiki ghorofa ya kupangisha katika manispaa mnayoishi. ...

Mkataba wa Kupanga

Kwa kawaida ghorofa ya kupangisha hupangishwa na manispaa husika, lakini wakati mwingine wakfu au mmiliki wa ...

Ankara

Kodi ya nyumba ya kupangwa hulipwa kila mwezi moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwenye nyumba. Kukosa kulipa ...

Sheria na Kanuni za Kawaida

Kwa kawaida mhamiaji anayekubaliwa na familia yake hupangisha nyumba ya kuishi katika jengo la nyumba nyingi ...

Taka

Kutunza usafi wa eneo la nyumba ya kampuni ni wajibu wa kila mpangaji. Mifuko yote ya taka lazima ipelekwe sehemu ...

Matengenezo ya Nyumba

Kila kampuni ya nyumba ina huduma zake za matengenezo ya nyumba, ambayo unawasiliana nayo iwapo mfereji, bakuli la ...

Maduka

Kuna duka au maduka mawili katikati ya kila Manispaa nchini Ufini. Kwa kawaida Wafini hununua chakula, mboga ...

Soko

Manispaa ya wastani na majiji yana soko ambapo unaweza kununua matunda na mboga, forosadi na samaki na ufurahie ...

Soko la Mitumba

Kumekuwa na ongezeko la mauzo ya mitumba hivi karibuni nchini Ufini. Masoko ya mitumba yana nguo nyingi za ...

Simu ya Mkononi

Kila mtu nchini Ufini; watoto, vijana, watu wazima na wakongwe ana simu. Unaweza kununua kadi ya simu ya malipo ...

Akaunti ya Benki na Kadi ya Benki

Ni muhimu kwa kila mtu mzima kufungua akaunti yake katika manispaa unayoishi au manispaa yaliyo karibu. Mtu hufungua ...

Usafiri wa Umma

Nchini Ufini kuna watu wengi wanaotumia usafiri wa kibinafsi, lakini watu wengine hutumia usafiri wa umma pia. Njia za ...

Basi

Watu husubiria mabasi kwenye vituo vya mabasi ambavyo vina ishara ya basi ambapo mabasi hupakia abiria. Basi ...

Garimoshi

Nchini Ufini kuna reli zinazomilikiwa na serikali na zinafanya kazi. Magarimoshi huenda sehemu mbalimbali nchini Ufini. Majiji ...

Baiskeli

Watu wengi hutumia baiskeli nchini Ufini. Watu wengi hutumia baiskeli wanapoenda shuleni au kazini. Baiskeli ...

Kuvuta Sigara

Sheria imepiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya umma; viwanja vya ndege, vituo vya magarimoshi, vituo vya ...




Majengo ya Kuishi katika Manispaa ya Makazi

Ghorofa ya Kupangisha

Kama sehemu ya msingi ya wahamiaji, wewe na familia yako mnastahiki ghorofa ya kupangisha katika manispaa mnayoishi. Ukubwa na idadi ya vyumba katika ghorofa yenu inategemea idadi ya wakazi, lakini vitu vya msingi katika ghorofa ya kupangisha havibadiliki.

Kwa kawaida nyumba ya kupangisha huwa na ukumbi, jiko, sebule, vyumba vya kulala, choo na bafu.

Vitu vya msingi vinavyopatikana jikoni huwa makabati, mfereji wa maji, karai ya kuosha vyombo, jiko la kupikia na oveni ya kuandaa chakula. Pia kuna friji na wakati mwingine mashine ya kuosha vyombo.

Kwa kawaida vifaa vya vyumba vya kulala na ukumbi huwa ni kabati la kuweka nguo na vitu vingine. Katika choo cha Ufini huwa na bakuli la kukalia na sehemu ya kunawa mikono. Vifaa ambavyo hupatikana bafuni huwa ni kifaa cha kutumia kuoga na kujikausha.

Kuna mtambo wa kuongeza joto katika ghorofa ambao huhakisha ghorofa inapata joto majira ya baridi. Kila chumba kina mtambo wa joto unaoweza kubadilishwa.

Mkataba wa Kupanga

Kwa kawaida ghorofa ya kupangisha hupangishwa na manispaa husika, lakini wakati mwingine wakfu au mmiliki wa kibinafsi. Mwenye nyumba na mpangaji hutia sahihi mkataba wa kupanga, ambao hufafanua kodi na muda wa kupanga. Mkataba wa kupanga huwataka wahusika kutii mkataba. Kwa kawaida nyumba za kupangisha huwa hazina samani yoyote. Ili uweze kuipamba unavyotaka wewe na familia yako.


Ankara

Kodi ya nyumba ya kupangwa hulipwa kila mwezi moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwenye nyumba. Kukosa kulipa kodi hubatilisha mkataba wa kupanga nyumba. Mbali na kodi inayolipwa kuna kodi ya maji ambayo hulipwa kando na hutegemea na idadi ya watu katika nyumba. Kodi ya maji hugharimia matumizi halisi ya maji, iwapo maji yatatumika zaidi kutakuwa na ada tofauti. Lazima wapangaji watie sahihi mkataba na kampuni ya umeme.

Ankara ya umeme hulipwa kila mwezi au mara nne kwa mwaka moja kwa moja katika akaunti ya kampuni ya umeme. Ukubwa wa kodi ya umeme hutegemea matumizi ya umeme katika nyumba iliyopangishwa. Ni muhimu kuzingatia matumizi ya maji na umeme, ili kuepuka gharama za ziada.


Sheria na Kanuni za Kawaida

Kwa kawaida mhamiaji anayekubaliwa na familia yake hupangisha nyumba ya kuishi katika jengo la nyumba nyingi linalomilikiwa na kampuni ya makazi yenye majengo mengi. Kila mtu anayepangisha nyumba ya kampuni lazima atii sheria na kanuni za kampuni inayomiliki nyumba hiyo. Hali ya utulivu inafaa kuzingatiwa kati ya saa 10 usiku na saa 7 asubuhi.

Chumba cha kufulia nguo katika nyumba kinaweza kutumiwa kwa muda tu uliowekwa. Gari linafaa kuegeshwa katika sehemu ya maegesho pekee. Kadhalika, wanaopanga nyumba wana jukumu la kuhakikisha usafi wa mazingira na kuzoa taka. Iwapo utakiuka kanuni hizi, majirani watawasilisha malalamiko yao kwa meneja wa kampuni inayomiliki nyumba.

Taka

Kutunza usafi wa eneo la nyumba ya kampuni ni wajibu wa kila mpangaji. Mifuko yote ya taka lazima ipelekwe sehemu maalum ya kutupa taka. Kuna sehemu za kutupa taka katika kila ua wa kila jengo, na wanaopanga wanapaswa kupeleka taka huko.

Kampuni nyingi za nyumba za makazi zina sehemu tofauti kwa kila aina ya taka. Wapangaji wanapaswa kupanga taka na kuitupa sehemu mwafaka. Kwa kawaida kuna jaa tofauti la taka ya karatasi, kadibodi na taka viumbe hai. Baadhi ya kampuni za nyumba zina makasha ya kutupia taka za glasi na chuma. Taka nyingine zote huwekwa kwenye jaa la kutupa taka.


Matengenezo ya Nyumba

Kila kampuni ya nyumba ina huduma zake za matengenezo ya nyumba, ambayo unawasiliana nayo iwapo mfereji, bakuli la chooni, au mtambo wa joto unahitaji kukarabatiwa. Ukigundua maji yanavuja katika nyumba, piga simu kwa huduma ya matengezo. Lazima upige ripoti kwa mwenye nyumba kumwarifu kuhusu uharibifu wowote utakaofanyika kwenye nyumba uliyopangisha. Mwenye nyumba anawajibishwa kukarabati au kubadilisha kifaa kilichoharibika kama vile friji, jiko na mfereji. Iwapo uharibifu umesababishwa na mpangaji, atalipia.

Kununua Bidhaa na Kutembea katika Manispaa

Maduka

Kuna duka au maduka mawili katikati ya kila Manispaa nchini Ufini. Kwa kawaida Wafini hununua chakula, mboga na matunda katika maduka makubwa na maduka ya jumla. Katika maduka ya jumla kuna maduka ya nguo na maduka ya viatu. Bei huwa tofauti katika maduka mbalimbali. Unaweza kupata taarifa kuhusu tofauti ya bei kutoka kwa watu ambao wameishi sehemu hiyo kwa muda mrefu. Unapoingia dukani unaweza kuchukua kigari au kikapu cha kuweka bidhaa utakazonunua.

Maduka haya ya jumla yana vitengo mbalimbali kwa kila aina ya bidhaa. Katika sehemu ya mboga na matunda unaweza kuchukua kiasi cha mboga na matunda unayotaka kwenye mfuko wa karatasi. Baada ya kuyachukua weka matunda au mboga hizo kwenye mizani, kisha bonyeza kitufe cha nambari ya bidhaa na mashini itakuonyesha bei yake. Unaweka tagi ya bei kwenye upande wa mfuko. Mkate huchukuliwa kutoka kwenye saraka ya mkate. Kwa kawaida samaki na nyama huagizwa kutoka kwenye kaunta iliyotengwa kwa bidhaa hiyo. Pia kunaweza kuwa na nguo na viatu vinavyouzwa dukani na tagi za bei zao zitakuwa zimepachikwa kwenye bidhaa hiyo. Unalipia bidhaa kwenye kaunta kwa pesa taslimu au kadi ya benki. Katika maduka ya Ufini kila mtu hujiwekea bidhaa alizonunua kwenye mifuko.

Katika manispaa kubwa na za kati na majiji unaweza kupata maduka ya vyakula yanayomilikiwa na wahamiaji. Katika maduka hayo utapata vitu vya kuungia chakula, masala na mboga nyingine unazohitaji ili kuandaa vyakula vya asili mbalimbali. Kupata fursa ya kuandaa na kufurahua chakula unachokifahamu hufanya maisha yawe ya starehe unapoishi ugenini. Ulizia maduka yanayomilikiwa na wahamiaji katika manispaa yako na maeneo ya karibu. Siku hizi kuna ofisi za posta katika maduka mengi, ambapo unaweza kutuma na kupokea barua na vifurushi. Kuna ofisi za posta za kujitegemea katika manispaa ya wastani na majiji.

Soko

Manispaa ya wastani na majiji yana soko ambapo unaweza kununua matunda na mboga, forosadi na samaki na ufurahie kahawa na watu wengine. Soko hufunguliwa kuanzia majira ya machipuko mpaka majira ya mapukutiko, na hufungwa wakati wa majira ya baridi kwa sababu ya hali ya baridi.


Soko la Mitumba

Kumekuwa na ongezeko la mauzo ya mitumba hivi karibuni nchini Ufini. Masoko ya mitumba yana nguo nyingi za watoto na watu wazima, na vifaa vya nyumbani, fanicha na toi za watoto ambazo ziko katika hali nzuri na ubora wa juu. Hasa nguo za watoto wachanga zinapatikana kwa wingi. Tembelea maduka ya mitumba yaliyo karibu kabla ya kununua bidhaa mpya. Ukinunua bidhaa za mitumba utaokoa hela nyingi ya matumizi ya nyumbani.


Simu ya Mkononi

Kila mtu nchini Ufini; watoto, vijana, watu wazima na wakongwe ana simu. Unaweza kununua kadi ya simu ya malipo ya kabla kwenye duka lililo karibu la R-kiosk au unaweza kupata kadi ya simu kutoka kwenye kampuni ya simu na ulipe bili ya kila mwezi.

Akaunti ya Benki na Kadi ya Benki

Ni muhimu kwa kila mtu mzima kufungua akaunti yake katika manispaa unayoishi au manispaa yaliyo karibu. Mtu hufungua akaunti ya benki kwa kutuma barua ya maombi. Kigezo cha kufungua akaunti ni kuwa na pasi halali, kibali cha kuishi na usajili katika manispaa.

Pindi tu akaunti inapofunguliwa utapata kadi ya benki ya binafsi. Unaweza kutumia kadi yako ya benki kutoa pesa kwenye mitambo ya ATM na uitumie kulipia bidhaa unazonunua dukani. Hakikisha unakumbuka PIN ya kadi yako ya benki. PINni tarakimu nne ambazo utapewa na benki yako. Kuna mitambo ya ATM katika kila kituo cha biashara na soko. Unaweza kutoa pesa kwenye mitambo ya ATM, kwa Yuro, ambayo ndiyo sarafu inayotumika nchini Ufini na nchi nyingine za Ulaya. Mtambo wa ATM ni kama kompyuta ndogo. Unaweza kutumiwa na PIN pekee. Weka namba yako ya siri katika mtambo wa ATM na kisha utoe pesa kwenye akaunti yako mwenyewe. Ni muhimu kulinda PIN yako na kadi yako ya benki zisipotee. Njia ya malipo inayotumika sana Ufini ni kutumia kadi ya benki. Unatia kadi yako ya benki kwenye mashine ndogo iliyopo dukani kisha uandike PIN yako. Malipo ya bidhaa ulizonunua yatakatwa moja kwa moja katika akaunti yako. Pia unaweza kulipa kwa hela taslimu.

Usafiri wa Umma

Nchini Ufini kuna watu wengi wanaotumia usafiri wa kibinafsi, lakini watu wengine hutumia usafiri wa umma pia. Njia za usafiri wa umma ni pamoja na mabasi, na magarimoshi. Pia kuna reli ya chini ya ardhi katika mji mkuu. Kwa safari za mbali njia za usafiri ni mabasi na magarimoshi. Kwa kawaida usafiri wa umma ni nafuu kuliko wa kibinafsi.


Basi

Watu husubiria mabasi kwenye vituo vya mabasi ambavyo vina ishara ya basi ambapo mabasi hupakia abiria. Basi linapokaribia kituoni mwonyeshe dereva ishara ya kusimama. Katika manispaa mengi nauli hulipwa kwa kutumia kadi ambayo abiria huwa ameweka pesa kabla. Kama huna kadi ya basi unalipa pesa taslimu. Mabasi ya safari za mbali hupakia abiria kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya mabasi ya safari za mbali. Nauli ya safari za mbali huwa nafuu kama utanunua tiketi kabla ya safari.

Garimoshi

Nchini Ufini kuna reli zinazomilikiwa na serikali na zinafanya kazi. Magarimoshi huenda sehemu mbalimbali nchini Ufini. Majiji yote ya wastani yana vituo vya reli. Magarimoshi husimama kwenye vituo vya magarimoshi ambapo abiria huabiri na kushuka. Kwa kawaida tiketi hununuliwa kwenye kituo cha garimoshi lakini zinaweza pia kununuliwa ndani ya garimoshi au mtandaoni.


Baiskeli

Watu wengi hutumia baiskeli nchini Ufini. Watu wengi hutumia baiskeli wanapoenda shuleni au kazini. Baiskeli huegeshwa sehemu ambazo zimetengewa. Unapoendesha baiskeli, ni muhimu kufuata sheria za barabarani na uvae helmeti. Anayeendesha baiskeli lazima ajali wanaotembea na wanaovuka barabara.

Kuvuta Sigara

Sheria imepiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya umma; viwanja vya ndege, vituo vya magarimoshi, vituo vya mabasi, ndani ya mabasi, ndani ya garimoshi, ndani ya ndege, shuleni, ofisini, njia za kumbi, mikutanoni. Kuna sehemu za umma zilizotengwa kwa ajili ya kuvuta sigara. Zimewekwa alama inayoonekana kwa urahisi. Mabaki ya sigara sharti yawekwe kwenye jaa lake.

Pakua hapa yaliyomo katika kurasa huu katika muundo wa PDF.